Nimeona na Mimi nije kuwaomba ushauri napitia changamoto kubwa ila naomba unifichie jina langu, positi tu huu ujumbe wangu.
Ukweli niseme Mimi kazi yangu ni kujiuza, nilianza kujiuza nilivyo maliza kidato Cha 4 mwaka 2015, niseme tu ilikuwa ni tamaa tu ila sikuwahi kufikiria kama nitakuja kujuta kiasi hiki.
Nimejiuza Sana na kusafiri mikoa mingi, nimetumika Kila sehemu, najua unaelewa nikisema Kila sehemu, yani najiona siyo binadamu tena, Sina thamani yoyote na najiona dhambi nilizo nazo hata sistahili kusamehewa.
Mwaka 2023 kaka zangu walikuja kugundua kuwa najiuza, walivyo gundua hivyo waliumia sana Kwa Sababu ni watu wenye kipato kizuri tu, wakanitafuta Kwa uchungu mkubwa sana wakaniambia nirudi nyumbani mkoani kwetu wanifungulie Biashara.
Nilikubali kurudi kweli, walinifungulia Biashara ya Grocery na wakaniwekea na Huduma za kipesa, wakaniambia kwenye hiyo Biashara nisiwe natumia pesa yoyote Mpaka ifike miezi nane, wakawa wananipa pesa ya Matumizi, ila pesa ya Biashara yangu nikawa naweka tu.
Sasa sijui shetani alikuja kunipitia tena nikaanza kujiuza hapo hapo, mara nikawa nafunga Biashara naenda gesti, mara narudi Dar Kwa wateja zangu nilio waacha, Yani nikawa naweza kumaliza wiki huku Biashara nimeifunga,
Kaka zangu walikuja Waka kasirika sana wakafunga Biashara wakanifukuza mana habari zilikuwa zimesha sambaa kuwa najiuza pale.
Ilibidi nirudi tena Dar kuendelea kujiuza mpaka Sasa, ukweli nimechoka sana, hata pesa nikipata sijui hata inaishia wapi.
Nimesha jaribu kufungua Biashara kupitia pesa ninayo ipata humu lakini Biashara inakufa tu unajikuta unarudi tena kujiuza.
Kuna kipindi nilijiuza sana Ili nipate pesa ninunue kiwanja, kweli nikanunua kiwanja lakini huwezi amini nilikuja Kuambiwa kiwanja kipo Katikati ya barabara pale chanika wakati nilikinunua kimepimwa na hakiko Katikati ya barabara, mpaka Sasa kweli barabara imepita Katikati ya kile kiwanja.
Najiuliza Mimi itakuwaje ndugu wote wamenitenga, hapa Dar naishi Mimi kama Mimi na marafiki zangu tu, najichukia sana, hakuna kitu kinauma kama usipo lala na mwanaume huwezi kula Wala kuvaa, hicho kitu kinaniuma sana.
Naumia sana kuona dada zangu wame Olewa na Wanafanya Biashara na waume zao halafu Mimi na umri wangu huu wa miaka 30 sijui kesho yangu ikoje, natamani kuacha ila nashindwa Mimi.
Tags:
Hadithi zetu