Tulibahatika kuzaa watoto watatu tukiwa kwenye nyumba ya kupanga badae Mungu alitujaalia tukapata kiwanja ila yeye hakuwa na pesa mimi ikabidi nilipie kwa madai atanirudishia nusu, ila hakuwahi kufanya hivyo tuliandika majina yetu wote basi miaka ikaenda hela sipewi nikauchuna tu kwavile sisi ni wanandoa na tunawatoto nikauchuna
Tukaanza ujenzi asilimia kubwa nilichangia mimi yeye kila siku hela hana, tukaezeka ila ikawa bado kusakafia, kupiga plasta, kuweka ceiling board, umeme na vingine vidogo vidogo, kila nikisema tuhamie mwanaume hataki mpata tukamilishe ukapita mwaka mambo bado na alinizuia kabisa kuwa naenda kule madai yake atamalizia palipobaki tuhamie mimi sawa, mwaka wa pili aaaa nikasema usinitanie nikategeshea kasafiri nikasema akirudi hanikuti hapa na hivi kodi ilikuwa mwishoni nikasema safii
Alivyosafiri tu nikaenda kuchukulia watoto uhamisho mmoja alikuwa la 3 mwingine la 1 wa mwisho alikuwa na miezi 6, nikamwambia hela ya kodi siku zimeisha ooooooh kesho nakutumia nikatulia alipotuma hiyo kesho yake nikaita gari pakia kila kitu huyo kwenye mjengo wangu, Ile nimefika naona kuna kama watu wanaishi hata sikujali kwa sababu hati ninazo mimi na pale najua kabisa ni kwangu nikawaambia niliokuja nao haya shusheni vitu ingizeni ndani si ndiyo anatoka mdada!
Bila hata salam, eti mnaingia tu kwenye majumba ya watu hamgongi hata hodi haya ondoeni vitu vyenu mtakuwa mmekosea nyumba hapa naishi mimi na mume wangu, nikamwambia labda nikuulize wewe ni nani kwenye nyumba yangu? Maana hapa ni kwangu na ndiyo nimehamia kama vipi muite huyo mumeo tuelezane vizuri akanijibu nyodo huyo akaingia ndani akafunga mlango
Wale wakaka wanaendelea kushusha vitu huku nampigia cm mume wangu hapatikani, nikaona nibebe vielelezo vyangu niende kwa mwenyekiti, nimeenda nimerudi na mwenyekiti anagongewa atoe hati eti anayo mume wangu na kasafiri ikabidi aulizwe mumeo ni nani? yani huwezi amini ile kutaja jina tu mimi nikaitika abee
nacheka kama mazuri
Ikabidi nimuulize tu kwa upole huyo mumeo mmefunga ndoa? Eti ndiyo, alikwambia ana mke? Hapana! Nikamwambia mpigie, hapatikani ikabidi nimpe hati asome naona mtu analia kama kafiwa, mwenyekiti akamwambia nadhani umeelewa sasa mpishe mama aingize vitu ndani we mtafute mumeo akutafutie kwako, mi nikamuuliza umehamia lini hapa eti mwaka jana na hapo kila kitu tayari ameshaweka
Basi ikabidi wale niliokuja nao waanze kazi ya kutoa vitu nje ili vyangu viingie ndani, kazi ikaisha nikatulia na wanangu yeye yupo nje analia mume hapatikani mara namuona shem nae, ila ndugu wa mume wanafki sana aisee, eti shem kwani kaka hakukwambia kama kaongeza mke na hapa inabidi muishi wawili? Aisee fanyeni kama mnaona nilimfurumushia mvua za mawe hatokaa asahau na yule mwanamke nikamtimua kabisa sitaki kumuona pale, akabeba nguo akaondoka vitu akaacha wala sikujali
Kama wiki hivi namuona mume huyo aisee nilimtokea na kisu mbona kumbe kaja na familia yake na huyo mkewe, niliwaambia kabisa sitaki kumuona yeyote hapa labda mje nimekufa la sivyo mtasababisha niende jela wanangu wabaki wanateseka, si ndiyo mama mkwe akaanza kuongea, eti mwanangu msamehe mumeo kateleza na maneno mengine kibao tu eti mpokee mke mwenzio muishi hapa wote, kauri yangu ilikuwa moja tu ondokeni kabla wakurya kichwani hawajapanda la sivyo nitamwaga damu ya mtu hapa, naona wameganda tu
Nikalusha kisu kwenye kukwepa kikampata mama mkwe mguuni mbona walikokotana hata sijui walitokomea wapi, tangu siku hiyo cm za msamaha haziishi, mpaka leo mwaka wa 4 sijapewa talaka, nipo busy nalea wanangu na kufanya kazi zangu na sitaki ndugu yeyote wa mume wala huyo mume nyumbani kwangu na huyo mkewe nasikia aliondokaga oman
Tags:
Kisa na Mkasa
