"Kuna watu Facebook wana tumia majina yangu na Wana Ingiza sana pesa kutumia hizo account.
Wanaume wengi huko wana tapeliwa, wana ombwa pesa ya Kusuka wana tuma, pesa ya kula wana tuma, halafu wakiuliza tukutane wapi Wana ambiwa waje Magomeni kagera ofisini kwangu.
Sasa wakifika wanaanza Kunilalamikia Mimi mpaka wengine wana tishia kunipiga.
Sasa niwaambie, Mimi Facebook sawa natumia ila huwa sijibu meseji huko na wala Sichat, hata TikTok huko sijibu meseji labda Instagram tu na account yangu ina tick ya blue
Jamani naombeni mnielewe Mimi asili yangu siyo ya kuomba omba hela Kwa Wanaume, najitafutia mwenyewe"
Hivi Kuna watu huwa wakiombwa kitu mtandaoni hata kama hawajakutana Wana tuma?
Tags:
MASTAA
