TAARIFA KWA UMMA
Kuanzia kesho yani Oktoba 15, 2026 Watanzania wote wapenda Haki bila kujali dini wala itikadi za Vyama tunaunganisha mioyo yetu katika FUNGA SALA/DUA NA MAOMBI KWA SIKU 21.
KUMUOMBA MUNGU ALIETUUMBA WANADAMU WOTE AAMUE MWENYEWE KATIKA HUKUMU YA TUNDULISSU
KUMBUKA SHERIA IKIPINDISHWA NA KUMUUMIZA MJUZI NA MTUNZI WA SHERIA ITAKUWA HATARI ZAIDI KWETU TUSIOJUA SHERIA.
HUKUMU YA TUNDULISSU NI HUKUMU JUU YA HAKI, KWELI, DEMOKRASIA NA MADAI HALALI KABISA .
TAFADHALI USIACHE KUSHIRIKI KATIKA HILI.
1. "Kwa wanadamu hili haiwezekani, kwa Mungu yote yawezekana"
> Mathayo 19:26
> "Yesu akawaangalia, akawaambia, Kwa wanadamu hayo hayawezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana."
2. "Hii haitoki ila kwa kufunga na kuomba"
> Mathayo 17:21
> "Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga."
Zote zina nguvu sana kwa mfungo wetu huu. Tunafunga na kuomba kwa jambo ambalo macho ya mwanadamu yamelishindwa, lakini kwa Mungu linawezekana.
