Mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, Damas Mgaya mwenye umri wa miaka 38 amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba chake, huku ikielezwa kuwa alijiny0nga kwa kutumia kamba ya kiatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga amethibitisha tukio hilo lililoripotiwa leo, Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi, akieleza kuwa Marehemu alikutwa akiwa na kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha.
Kwa mujibu wa Kamanda Banga, tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na msongo wa mawazo uliotokana na mgogoro wa kifamilia kati ya Marehemu na Mkewe, ikiwemo kutokubaliana kuhusu kushiriki tendo la ndoa, ambapo inadaiwa Mkewe alikuwa akikataa kwa sababu yeye alikuwa ameokoka Kwa Yesu na mumewe alikuwa hajaokoka
<<<
Sasa wanawake na nyie aisee
Tags:
Maisha