Dalili 5 kwamba unamchagua mwenza kwa sababu ya upweke
Wakati mwingine mtu anaingia kwenye mahusiano si kwa sababu amempata mtu anayemfaa, bali kwa sababu amechoka kuwa peke yake. Hali hii inaweza kumfanya achague mtu asiyelingana na mahitaji yake ya kihisia na maisha yake.
Hizi ni dalili 5 za kuangalia:
1. Unaogopa kukaa bila kuwa na mtu.
Unahisi maisha yako hayajakamilika kama huna mpenzi. Hata kama hujafurahia mahusiano yaliyopo, unaendelea kuyashikilia kwa sababu unaogopa kurudi kuwa single.
2. Unakubali mambo ambayo hukupaswa kuyavumilia.
Unavumilia dharau, uongo, kutokujaliwa na hata kutoheshimiwa kwa sababu unaogopa kumpoteza mtu huyo.
3. Unampenda mtu kwa sababu anakupa attention.
Hujajua vizuri tabia, misimamo na malengo yake, lakini kwa sababu anakutafuta, anakupigia simu na kukupa muda, unaanza kumwona kama mwenza sahihi.
4. Unaharakisha mahusiano bila kumfahamu vizuri.
Baada ya muda mfupi tu, tayari unafikiria ndoa na maisha ya pamoja. Unatanguliza hamu ya kuwa na mtu kuliko kujenga uelewa wa kweli kuhusu huyo mtu.
5. Unachagua mtu yeyote anayekuonyesha upendo.
Badala ya kujiuliza kama mnaendana, unajiuliza kama anakupenda. Unasahau kwamba kupendwa na mtu si lazima kumaanishe kwamba mtu huyo anakufaa.
Funzo muhimu
Usiingie kwenye mahusiano kwa sababu tu umechoka kuwa peke yako. Jifunze kufurahia maisha yako hata bila mwenza. Mahusiano mazuri yanapaswa kuongeza thamani katika maisha yako, si kuwa njia pekee ya kukufanya ujisikie mwenye thamani.
Swali la mjadala:
Je, ni bora kuwa single ukiwa na amani au kuwa kwenye mahusiano ambayo yanakunyima amani?
Urafiki • Uchumba • Ndoa
