NI VIZURI WANAWAKE MKAFAHAMU HILI, NI NGUMU SANA MWANAUME AMUACHE MKE WAKE WA NDOA ILI AKUOE WEWE.
Wasichana na wanawake nataka mfahamu hili. Ni ngumu sana mwanaume amuache first wife (mke wake wa ndoa) ili akuoe wewe. Ni ngumu sana huwa tunawadanganya tu hivyo kwa kuwa hampendi kuambiwa UKWELI ili tuendelee kuwatumikisha kingono (sex). Katika wanaume 1000 ni 1 pekee huchukua maamuzi haya magumu na tafiti zimeonesha wanaume walioacha wake zao wa ndoa wakaenda kuoa mchepuko, huo huo mchepuko huwa ndio chanzo chake cha kifo.
Wakati mwingine huwa inatubidi tuwadanganye tu kwa kuwaambia UONGO kuwa wake zetu hawajui mapenzi, hawatumii mtandao wa Tigo ili ninyi mtumie UDHAIFU huo kutupatia mapenzi motomoto mbinuke hadi mnavunja vitanda huku mkitupatia huduma ya Tigo. Lakini UKWELI ni kwamba wake zetu tunawaheshimu na kuwapenda sana na kwa kuwa pia tunapenda Tigo hatuwezi kuwavunjia heshima hivyo tunawatumia tu ninyi kupata huduma hizo na nyingine nyingi kwenu.
Hata hivyo asilimia 99 ya wanaume walioacha wake zao na kwenda kuoa mchepuko basi ukifuatilia vizuri unakuta haikuwa AKILI timamu ya mwanaume bali mchepuko ulitumia nguvu za GIZA (uchawi) kuteka AKILI ya mwanaume akajikuta anachukua maamuzi akiwa hajitambui. Na mwanamke wa hivi huwa hajampenda mwanaume bali kuna kitu kakipenda kwa mwanaume yaweza kuwa pesa, mali au mafao ya kustaafu na akishapata akitakacho humuua huyo mwanaume. Hili halina mjadala liko wazi halihitaji kubishaniwa. Waliowaacha wake zao kwa tamaa za nyumba ndogo walipata faraja ya muda mfupi tu kisha wakafa kifo cha mateso makali kilichoratibiwa na nyumba ndogo ili abaki HURU akifurahia mali na pesa ulizompelekea huku watoto na mke wako wakiteseka.
Nimalizie kusema kuwa kama wewe unatembea na mume wa mtu ukiitarajia ndoa kwa ushawishi wa mahaba yako tu utabinuka mpaka uchakae na mwisho wa siku mwanaume ataendelea na familia yake. Ikiwa unataka akuoe uwe tayari kuchukua njia ngumu na mbaya ya kumteka kichawi na ukishamchukua mateka ukapata ukitakacho umuue au kumfanya zezeta kabla hajashtuka ukakosa mwana na Maji ya MOTO.
Na hiyo nguvu yote ya kufanya hayo si utafute tu mume wako hata kama hana kitu mutafute naye ili awe na mali na pesa unazozitamani?
Na ewe mwanamke kabla hujachukua uamuzi wa kishetani wa kuchukua mume wa mtu jiulize kwanza kuhusu mateso huyo mwanamke mwenzako atakayoyapitia je wewe ungetamani uyapitie au ungejisikiaje ikiwa ni binti yako anafanyiwa hayo?
Je umejiuliza namna ambavyo watoto wake watakavyonyanyasika na kuteseka kwa ajili yako?
Hupendi kukitendewa basi na wewe usimtendee mwenzako. Adui wa mwanamke ni mwanamke. Adui wa kwanza wa ndoa ni mwanaume mwenyewe
0 Comments