Habari zenu marafiki zangu wa jarida la Urafikihadindoa. Nikushukuru kwa kuchukua nafasi yako ili uweze kuisoma kwa uzuri makala hii ambayo najua vijana wengi walikuwa na shauku ya kutaka kuifahamu.
Bila kupoteza muda twende kwenye somo letu la leo; tuanze na maana ya kutongoza tunaweza sema ni kumshawishi mtu hasa jinsia nyingine ambaye hana uhusiano wowote wa kifamilia ili aweze kuwa mpenzi wako au aweze kuwa mwandani wako wa maisha.
Wengine wanasema kutongoza ni namna ya kuziuza sera zako ili ziweze kukubaliwa na mwenzako. Unajua tutnatoka kwenye tamaduni tofauti tofauti na kila mmoja ana miiko yake anayoijua. Mara nyingi tunasema mwamaume ndio anaye weza kumtongoza mwanamke au binti.
Kuna baadhi ya sehemu mwanamke naye pia anaweza kumtongoza mwanaume. Lakini twende na somo letu la siku ya leo.
Unaweza kujijengea dhana kwamba naweza kukubaliwa au kukataliwa, sasa majibu yote yatatokana na muhusika kwani kupata na kukosa pia ni kawaida katika hizi mishemishe za kutongoza.
Tuanze na dhima kubwa ya kutongoza ni ushawishi; unaweza kuwa wa pesa, fahari, mwonekano hata mvuto ambao unauhitaji. Lakini sio kila mmoja anapenda pesa au mwonekano, wengine ni muda umefika na wengine wanataka wapate watu watakao wajari au kuwathamini. Kuna wengine ni kwa sababu ya kuzichochea tamaa zao ndio utakuta akiona kila mwanamke anataka awe wake. Pengine ni tamaa za mwili zinamsukuma au ndio haiba yake hiyo.
Ili uweze kumtongoza mwanamke yeyote yule na ukafanikiwa kuna mambo ya kufanya na pia kuna mambo ambayo unatakiwa uyajue.
Mambo unayotakiwa uyajue kabla ya kutongoza;
- Ni wakati gani naweza kuongea kusudio langu?
- Je mwenzangu yupo katika hai gani sasa?
- Mtazamo wake ni upi?
- Je, huyu naweza kumfuata?
- Je huyu tunaendana?
0 Comments