Hata kama una uzuri kiasi gani ila tambua kwamba huwezi kupendwa na kila mtu.



Nikuambie tu ukweli:kuna wengine wana tamaa tu juu yako na usipokuwa makini utadhani wanakupenda.
Mwisho wa siku unajikuta unaachana na yule mwenye upendo wa dhati na kwenda kwa yule aliyekutamani.
Ukija kushtuka unakuta tayari muda umeenda na yule aliyekupenda tayari ana maisha yake mengine.
Kuwa makini na watu wanaohitaji mapenzi nawe.
Kuwa na jicho la tofauti na utumie akili kumjua yule aliye sahihi na uwakwepe wenye kukutamani au kutamani vitu vyako.